Msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto
amedai kuwa ajisikii vizuri pindi anapo vaa viatu kutokana kudai kuvaa
viatu kuna athiri utendaji wa kazi zake.
Mpoto ameiambia bongo5 kuwa amesemwa sana kuhusu tabia ya kuto vaa viatu lakini ameshindwa kubadilika.
“Beauty yoyote ipo kwenye
jicho,unapozungumzi Mrisho Mpoto kuwa peku ,sehemu nyingi sana,mara
nyingi sana watu wananiona peku, ni kwa sababu ya kutafuta energy
,unajua energy ya mimi kuendelea kuishi inapatikana kwenye udongo,yani
ngozi yangu inapokutana na ardhi nakuwa so (confident) na nakuwa Mpoto,
zaidi na nguvu na nakuwa na akili ,sasa sipendi wakati mwingine kuwa
fake,najitaidi sana kuwa wakisasa ila nakuwa nasahau,kwamfano naweza
nikanunu kiatu cha gharama alafu nikakisahau kwenye ndege au kwenye basi
kwasababu siyo kawaida yangu kuvaa viatu, nisha jaribu lakini
nimeshapoteza vingi,kwasababu siyo culture yangu kuvaa viatu ,viatu
navaaga kwasababu watu wananisema.kwaiyo nikivaa ninakuwa kama
inanisumbua, nikaona kama bora niache,alafu nakuwa siko huru,ukinikuta
nimevaa viatu alafu tukaanza kufanya mazungumzo nakuwa siko huru
kwasababu nakuwa nipo kama naelea hewani,yani kama sina chaji,kwaiyo
kwangu mimi ardhi ni kama plug ya mwili wangu,nikikanyaga chini wewe
niulize chochote nitakujibu niambie niandike shairi la haina yoyote,mimi
ata nikiandika nyumbani kwangu lazima niweke miguu kwenye mchanga,ata
nyumbani kwangu hakuna mchanga mimi ninabeseni kabisa la
michanga,kwajili tu yakukanyaga yani nikiandika nakuwa confidant ata
nikiandika nakuwa na amani”Alisema Mpoto
Pia Mrisho ataendelea kufafanua kwanini ataki kubadilika na kuchana na tamaduni ya kutembea mbila kuvaa viatu
“Nataka maisha yasiniendeshe mimi,mimi
niyaendeshe maisha, kwasababu unajua speed ya utandawazi yani
globalization ni kubwa sana kuliko speed ya mwanadamu kwa
Tanzania,ukiangalia watu kama Marekani wamepata uhuru miaka mia mbili
iliyopita,sisi tuna miaka mingapi tu ya uhuru na teknologia inakuja kwa
kasi sana,ndiyo maana technologia inapokuta Tanzania watu wanaimasta
sana,kwamfano facebook,instargam,twetter,whatsapp na mitandao mingine
vimekuja kwa kasi sana na watu vimewabadilisha sana,ata Ngugi wa
Thiong’o alisema huwezi kwenda kwa jirani kama ujatokea kwako,mtu kaka
mimi ninapoigia kwenye technologia siwezi badilishwa kwasababu
nimeshajijua mimi ni
nani”Alimalizia Mpoto
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni