Jumatatu, 18 Novemba 2013

fahamu sababu kuu za mimba kuharibika.

Kuharibika kwa mimba ni tatizo linaloweza kumpata mwanamke yoyote.

Sababu za mimba kuharibika mara kwa mara kitaalam hazijulikan, ila kuna vyanzo vinavyojulikana kusaidia mimba kutoka. mbali na mimba zinazotolewa kwa njia haramu, sababu za zinazotoka bila kulazimishwa zinatajwa kuwa ni maumbile ya uridhi, kwa maana ya kuwa na vinasaba ambavyo si vyakawaida kwahiyo kiumbe kinakuwa katika hali ambayo kwa asili mimba haiwezi kukua.

MAUMBILE YAI.



Nikwamba mtoto akizaliwa atakuwa na matatizo ya kimaumbile na kiakili. Nikwasababu hiyo mimba huharibika na kutoka yenyewe. Sababu nyingine ni kutokuwepo kwa yai lililorutubishwa. Katika uumbaji, yai hukutana na mbegu ya mwanaume na mchakato wa kiumbe kukua huanza kwa yai kujitenga mara mbili. Upande mmoja hutengeneza kondo la nyuma na kifuko cha kutunza maji na sehemu ya pili hutengeneza mtoto.Inatokea kuwa sehemu ya kondo la nyuma inaendelea kukua wakati sehemu ya mtoto haikui kabisa
.

Ikiwa mama hajafanya vipimo vinavyoweza kuangalia maendeleo ya mtoto tumboni, atakuwa akifikiria kuwa ni mjamzito, kwani kwa wakati huo kipimo cha mkojo kinaweza kuendelea kuonyesha kuwa ni mjamzito. Hata ivyo kuna uwezekano wa mimba hiyo kutoka kabla ya kufikisha wiki 24. Ieleweke kuwa uvutaji wa sigara huchangia sana kuaribika kwa mimba lakini pia kunywa pombe kupita kiasi husababisha hali hiyo.

wengine huaribu mimba kutokana na kuwa na msongo wa mawazo na ukosefu wa viini lishe katika mwili . Lakini kuna baadhi ya magonjwa ambayo akiyapata mjamzito humdhuru mtoto aliye tumboni na kusababisha mimba kuharibika. Magonjwa hayo nikama  vile malaria, kaswende na kadhalika.

DALILI ZA MIMBA KUHARIBIKA.

Dalili za mimba kuharibika ni pamoja na mjamzito kutokwa na matone ya damu na kupatwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu bada ya kukosa siku zake kwasababu ya ujauzito.
Wajawazito wengine wanaweza kutokwa damu bila kuhisi maumivu ya tumbo kabisa. Asilimia kubwa ya mimba kuharibika katika kipindi cha awali kabisa cha ujauzito au ndani ya wiki 14 za ujauzito. Wengi wa wanawake ama kwa uwelewa ndogo au kudharau, kupuuza dalili za kutokwa damu hasa kama ni kidogo hivyo kuchelewa kwenda hospitali kuchunguzwa na matokeo yake ni mimba  kuharibika au kutoka.

USHAURI.


Iwapo mimba zitatoka bila kuwa na sababu inayojulikana inatakiwa mjamzito afanyiwe uchuguzi wa magonjwa ya uridhi na magonjwa mengine yanayosababisha mimba kuharibika. Ni vyema kila mwanamke akapata chanjo zote tano za pepopunda anapofikia umri wa kuzaa au anaposhika mimba.
Vipimo kama Ultrasound ni muhumu kufanyiwa mapema wakati wa ujauzito ili kuhakiki kama mtoo anakua ipasavyo. Matibabu ya kuharibika kwa mimba yanapatikana endapo utawahi kuchunguzwa. Lishe bora kwa mjamzito itazuia kuharibika kwa mimba na mtoto atakaezaliwa atakuwa na afya njema.

via Dk Rose.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni