Mama mzazi wa mwanafunzi anaedaiwa kubakwa, Mary Mkombola akisimulia tukio la ubakaji lililo mpata mwanae na kusababisha mimba mbele ya waandishi wa habari. Kulia ni Martha Daniel (17) anaesoma shule ya city secondary kidato cha tatu aliyefanyiwa kitendo hicho.
Mwanasheria mfawidhi mkazi wa kituo cha msaada wa kisheria Tanzania Legal Aid Centre(TALAC) Godwin Ngongi akifafanua jambo kitokana na kitendo alichofanyiwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Martha
kwa mujibu wa mama huyo alisema binti yake amekuwa akisumbuliwa na mapepo ivo akaamua kumpeleka kwa mchungaj kwa ajiri ya maombi.
Kwamujibu wa mama huyo baada ya mchungaji kumfanyia maombi aliahidi kumsomesha kwa kumlipia ada ya mwaka mzima kutokana na yeye kuwa mjane.
Aliongeza kuwa baada ya kukubaliana na mtoto wake walienda kutoa taarifa shuleni ambapo walisema aje na barua itakayoonesha kuwa atamlipia ada hiyo.
Mkombola alifafanua kuwa aliongezakuwa mara baada yakupeleka barua shule na kukubaliwa, ilibidi aendelee na shule lakini baadae alianza kuhisi ni mjamzito.
mama huyo alimuuliza mwanae kama ni mjamzito kutokana na kuona dalili lakini binti yake alikataa kumweleza ndipo nilipoamua kumchapa na kukimbilia kwa mama yake mkubwa maeneo ya mbwanga.
"Alipokimbilia kule ndipo alipowaeleza mama zake wakubwa kwamba mama ananipiga wakati mimba nimeipata kule alikonipeleka nifanyiwe maombi, Ilibidi wanipigie waniambie kuwa mwanangu ana ujauzito na kaupewa na nabii Elisha.
"Nilimuuliza akanisimuli mambo yote anayofanyiwa na mchungaji Elisha toka nimpeleke mwezi mach mwaka huu" Alisema...
Mama huyo alikwenda polisi kuripoti ambapo alipatiwa fomu ya matibabu ambapo binti alionekana ni mjamzito.
alisema alipeleka majibu hayo polisi ambapo walimwambia asubiri uchunguzi unafanyika na utachukua muda mrefu.
Alibainisha kuwa baada ya viongozi wa kanisa kupata taarifa walimfata mama huyo na kumsihi asipeleke swala hilo polisi wao watalimaliza.
"Walinifuata watumishi wawili ambao ni Nabii Mgamba na Nabii Monika wakasema nisifanye lolote wao watamtunza na kama ikiwezekana tuitoe mimba hii, jambo ambalo sikuafikiana nalo." Alisema
Nae mwanafunzi alisema kuwa juni 8 alipigiwa simu na Nabii Elisha akamwambia aende mjini na alipofika alimpakia kwenye gari na kwenda nae kwenye nyumba ya kulala wageni iliyo jirani na chuo cha CBE iliopo mjini hapa.
"Nilimuuliza tunakwenda wapi alinijibu kuwa tunakwenda kanisani lakini chakushangaza tuliipita kanisa hivyo nikawa na wasiwasi lakini kabla hatujafika tulipokuwa tunakwenda alipita sehemu akaongeza upepo kwenye tairi" Alisema
kwamba baada ya kuweka upepo, waliondoka na kwenda katika nyumba hiyo ya kulala wageni lakini kabla hawajashuka alimpati soda aina ya fanta akanywa kwamuda mfupi niliweza kupoteza fahamu kidogo na alipozinduka alikuta anafanya mapenzi na mchungaji huyo.
"nilijikuta kifuani mwa nabii sote tukiwa watupu, nikaanza kulia akanibembeleza na akanambia 'unafikiri kukulipia ada yote ni bure' mbona wapo wengi sijawalipia ada, lazima nifanye na wewe mapenzi mara tano, kwahiyo bado mara nne nitafanya na wewe hata kwa nguvu na ukimwambia mtu nitakuua kwa maombi" Alisema
Binti huyo alidai kwamba toka siku hiyo hakuwahi kuziona siku zake mpaka mama yake alipoanza kumhisi kwamba anaujauzito na kuamua kumpeleka kupima ambapo walibaini ni kweli.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alidhibitisha kuwa tayari amekwisha yapokea malalamiko ya mwanafunzi huyo na anayatendea kazi.
"Tunayafanyia kazi kwani tulipata malalamiko hayo lakini tunasubiri mpaka ajifungue ili tuweze kutumia kipimo cha vinasaba (DNA) kudhibitisha aliyempa ujauzito" Alisema
Alipotafutwa Nabii Elisha alisema kuwa hayupo Dodoma kwa wakati huu na kumtaka mwandishi aende polisi atapata maelezo zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni