Jumapili, 13 Aprili 2014

John de mkali: mapenzii hayalazmishwii.

.Natambua kuwa kila mtu anatafasiri/
tafsiri yake ya neno mapenzi au maana
halisi ya kupenda  Moyo
wako siku zote unajua pale
unapompenda mtu n ahivyo huitaji
kuulazimisha, kuushawishi au kuomba
ushauri kwa watu wengine kama itakuwa
sahihi kuwa na fulani au la!


Penzi na jinsi linavyojitokeza (Forms)
zake ni hadithi ndefu na inachanganya,
sote tunajua swala zima la mapenzi
linachanganya na halina kanuni lakini ni
moyo wako pekee ndio utakao jua kama
hapo "umefika bei" au la!

*Penzi tamu na mara nyingi hudumu kwa
muda mrefu ni lile lililo-base kwenye
urafiki. Urafiki mwema siku zote huwa
hauna mwisho hali kadhalika mapenzi
yakweli hayana mwisho sasa hebu
changanga pamoja uone matokeo.

Mnapokuwa marafiki kwanza
nakuzoeana sana kiasi kwamba
mnasaidiana vilevile mnakuwa huru au
wazi ktk kuzungumzia mambo binafsi
kama vile furaha, karaha,
matatizo,mafanikio namengine mengi
muhimu napengine kujua mapungufu
yenu ambayo kama marafiki mnakuwa
tayari mnajua jinsi ya kuishi nayo
aukuyavumilia na hivyo mnaendelea na
maisha yenu yenye furaha na amani
kama marafiki na wakato huohuo
wapenzi.

Tatizo la penzi lililojengeka ktk urafiki ni
kwa mmoja wenu kuhofia urafiki kufa
ikiwa ataziweka hisia zake wazi kwa
mwenzie. Ikiwa utamkataa ni wazi kuwa
itakuwa ngumu sana kwake kuvumilia
kukuona wewe kuwa na mtu mwingine
kama mpenzi na sio yeye.

*Penzi liloegemea kwenye kupendeza/
kuvutia hufa au hufikia kikomo mara tu
mmoja wenu anapobadilika au kutovutia
tena kutokana na sababu tofauti za
kimaisha. Ukitaka penzi libaki pale pale
basi ni wajibu wako kuendelea kuwa
hivyo ulivyo (kupendeza/kuvutia).
Nakumbuka juzi nikiwa kwenye “office
do” , Jamaa (nafanya nae kazi)
akinilalamikia kuwa “My wife didn’t look
like that when we met, she was so hot
like those women” (akionyesha
wanawake wenye maumbile mazuri na
wamependeza kimavazi)”
nikamuangaliaaaaa kisha nikamuuliza
unadhani hakuvutii tena?
Akasema “ndio, hata kufanya mapenzi
inakuwa ngumu siku hizi”. Nikamuuliza
tena huoni kuwa amekuwa hivyo alivyo
kwa sababu yako? Akauliza “kwanini”
nikamwambia hukumwambia wazi kuwa
unachopenda kwake ni “the way she
look, nothing more” angejua angefanya
uamuzi wa busara kuliko kufunga ndoa
na wewe na kisha kukuzaliwa watoto.
Nikamwambia the woman needed/needs
ur love and support!........(ni mfano ulio
hai ulionisukuma kuandika hii topic).

Penzi lisilo na mwisho ni lile linalijotokeza
kiasilia (naturally) kwamba unakutana na
mtu (sizungumzii love @ 1st sight hapa)
kisha mnajikuta mnapendana kwa dhati
penzi hili hunawiri vizuri sana na
hudumu kwa muda mrefu na ikitokea
mmoja kumuacha mwenzie basi itakuwa
ni sababu “nzito” ambayo ni kifo (ndio
pekee kitatenganisha penzi hili).
Atakae baki humuhuia vigumu sana
kuwa na mpenzi mwingine na
itamchukua muda mrefu sana
“kumdondokea” mtu mwingine “Bond”
ya penzi hili ndio wengine huita penzi la
kweli.

N:B Tafadhali tambua kuwa kuna tofauti
kati ya Kuvutiwa, Kupenda na kufaa
kuwa mke/mume japo kuwa wote
watakutamkia kuwa wanakupenda and
all lakini wengi huchanganya hisia za
mapenzi na zile za kutamani na wale wa

“anafaa” wao huchukua/chukuliwa jumla
wakidai “wamefika bei” ili kuridhisha
jamii lakini ukweli utaujua mbele kwa
mbele.Tafadhali ongezea maelezo, uzoefu wako
kuhusu penzi ili sote tujifunze, kumbuka
kujifunza hakuna mwisho na kila kukicha
tunajifunza au kukumbushana mambo
mapya, asanteni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni