Ni siku chache tu zimepita toka Paul
Okoye wa kundi la P-Square afanye harusi ya kimila na mke wake Anita
Isama huko Nigeria, lakini baada ya wote wawili (Peter & Paul)
kukamilisha majukumu ya ndoa zao, kuna habari ambazo zimesambaa wiki hii
kuwa umeibuka ugomvi baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao
inasemekana sasa hawaelewani vizuri.
Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa
kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa kumekuwa na kutoelewana baina ya
kaka mkubwa wa mapacha hao Jude Okoye na mke wa mdogo wake Peter Okoye
aitwaye Lola Omotayo, kitu kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao
mwaka jana.
Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi
ya Peter na Lola mwaka jana, lakini alihudhuria ya Paul na Anita mwaka
huu kitu kinachowafanya watu waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina yao.
Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa
ugomvi huo unaomhusu Lola umesababisha Peter na Paul kugombana wakati
wako kwenye rehearsle Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na
dancers wao.
Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na ugomvi wao.
“After over 10 years of hard work, it’s
over. (I) Am done.” ikiaminika kuwa alimaanisha amejiondoa kuli-manage
kundi hilo japo kuwa yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha katika
maneno hayo machache.
After over 10yrs of hard work, it's over. Am done.
— IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014
Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa
miaka yote na kuproduce hits zao paomoja na kudirect idadi kubwa ya
video zao zilizofanya vizuri.
Lakini kuna baadhi ya watu nchini
Nigeria wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na
kuripotiwa katika vyombo vya habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya
album yao mpya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni