HATIMAYE mwanamuziki wa kike nchini
Marekania Rihanna amethibitisha kutokuwa na mpango wa kurudiana tena na
aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Chris Brown baada ya kuweka wazi
mahusiano yake mapya aliyokuwa akiyaficha kwa muda mrefu sasa.
Rihanna amethibitisha kuwa na mahusiano
na mwanamuziki mwenzake Drake, ambapo wameamua kuyaweka wazi mahusiano
hayo na siyo ya kificho tena mara baada ya kuwepo na tetesi nyingi juu
ya mahusiano ya watu hao wawili.
Vyanzo mbalimbali vimeuambia mtandao wa
TMZ, kuwa Rihanna na Drake wameamua kuweka wazi uhusiano huo kwa kuwa
karibu zaidi huku mwanadada huyo kuamua kuvaa nguo za Drake.
Kama hiyo haitoshi tuu mwanadada huyo
ameamua kuonesha mapenzi hayo hadaharani kwa kumfuata hadi chooni huku
akiwa amevaa nguo ya mwanaume wake.
Vyanzo hivyo vimedai kuwa Rihanna
hutumia muda mwingi kwa kuwa na Drake kwa madai kuwa anamjali kuliko
aliyekuwa mpenzi wake wa awali..Wakati huo huo Chriss Brown anazidi
kuchanganyikiwa kwa kuona wawili hao wakiwa Ng'are Ng'are inadaiwa kuwa
amefanya vurugu Kule rehab hadi amefukuzwa na amehukumiwa kwenda jela
Mwezi mmoja
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni