KujamianLakini, kuna
a (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule.
faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, mwandishi wako Dk. Khamis Hassan anajaribu kutueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.
a (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule.
faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, mwandishi wako Dk. Khamis Hassan anajaribu kutueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.
KUMBUKA
Unapaswa bado kufanya mambo
mengine ili kwamba kufanya mfumo wako wa kinga na uwe imara, kama
vile: Kula vizuri, kufanya mazoezii, kupata usingizi wa kutosha,
n.k. Pia katika mapenzi matumizi ya kondomu kama hamjuani wote kuhusu
hali magonjwa ya zinaa yako baina yenu. Ili kujikinga na afya zenu kwa
kujiepusha na hayo magonjwa yanayoweza kushusha kiwango cha kinga ya
mwili wako.
1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo:
Wanawake ambao hufika kilele (orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30%
tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni
kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza
msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha
kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa
kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi. Uwezekano wa kupata
mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1
tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na
kujamiana. Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata
mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu
asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya
vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la
moyo wakati wa kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50,
uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza
kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.
2. Huongeza ukakamavu wa mifupa:
Wanawake waliokoma kupata hedhi
(menopausal women) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana
kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao
hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake
waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa
ujulikanao kamaosteoporosis.
3.Hupunguza msongo wa mawazo:
Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na
shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele
ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya
mwili kupumzika, musclerelaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini
watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza
kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo.
Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la
damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vyaprostaglandins
katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi
hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya
zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu
kwa afya njema.
4. Hupunguza maumivu:
Kufikia kilele (orgasm) wakati wa
kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi
kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza
maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili
zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post menopausal syndrome symptom).
5. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume:
Wanaume walio na umri wa miaka 50 na
zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata
saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha
tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati
wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo
wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa
ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.
6. Huongeza uwezo wa kunusa:
Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni
ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo (brain stem
cells) kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa na
kutambua harufu (brain olfactory bulb).
7. Hupunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema:
Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa
kujamiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka
150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu.
Kujamiana huchoma karibu 200 calories sawa na kukimbia dakika 15 katika
mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47
zaidi.
8. Huongeza kinga ya mwili:
Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili
kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina yaimmunoglobulin A kwa
robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.
9. Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke:
Wanawake wanaojamiana angalau mara nne
kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa
miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni
ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na afya nzuri na
ngozi zao kungaa.
10. Hudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida:
Wanawake ambao hujamiana angalau mara
moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko
wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa
nadra au wale ambao hawafanyi kabisa.
11. Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini:
Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.
12. Huongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles):
Na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo
ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata
hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa
sehemu za siri za mwanamke (vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na
maambukizi katika njia cha mkojo (Urinary Tract Infection ).
13. Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini:
Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko
wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya
oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo
kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.
14. Huongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako:
Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana
maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote hupatikana wakati mtu yupo
uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile
mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda kwa
binadamu yoyote.
15. Husaidia kuishi kwa muda mrefu:
Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa
wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA
(Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na
kufikia kilele. DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu
zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha
ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo.
Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha
yako.
16. Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi:
Kutokana na kuongezeka kwa homoni ya
oxytocin (love hormone), ambayo huleta mshikamano, uaminifu, na
unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.
17. Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba:
Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa
uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana!
Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya
kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora
kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa
siku nne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni