Sehemu ya Lori lililopata ajali
Edwin Moshi wa Eddy Blog
Watumiaji
wa barabara ya Iringa Njombe wamekwama toka jana majira ya saa 10 jioni
kufuatia ajali ya lori lililobeba shaba lenye namba za usajili T 261
BCM linalovuta tela lenye namba za usajili T 595 BAS kupata ajali na
kufunga barabara na kusababisha magari kushindwa kupita.
Mtandao
huu umeshuhudia msururu mkubwa wa magari yanayokwenda mikoa ya njombe
Ruvuma Mbeya na nchi jirani, pamoja na yanayotoka kwenye mikoa hiyo
kwenda Iringa Dodoma, Dare es Salaam na mikoa mingine yakiwa yamekwama
kwenye msururu huo.
Ajali hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa.
Ajali hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa.
Baadhi ya
abiria na madereva wa malori waliokuwa eneo la tukio wamelalamikia
ufinyu vya kulitoa lori hilo kuwa ni hafifu hali iliyopelekea wakae hapo
muda mrefu(karibia siku moja).
Hali hiyo iliondolewa majira ya saa tatu asubuhi baada ya lori hilo kufanikiwa kuondolewa barabarani na kusogezwa pembeni ndipo magari hayo yakaendelea na safari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni