Hapa sasa picha kamili inaonekana bila chenga kabisa hebu weka ushabiki pembeni alafu mtanielewa kwanza kumbukeni Lukuvi ni kiongozi wa juu kabisa wa serikali ukiachana na ujumbe wake ndani ya bunge maalumu la Katiba sasa kama ni taarifa za kiintelejensia atakua ameshazipata siku nyingi sana na ndio maana yeye kama mjumbe alitoa maoni yake kikamilifu na akaligusia hilo na kulifafanua bila uwoga kabisa maana hata ukimuuliza hana wasiwasi na anakuhambulia kimoja kimoja.
Napata mashaka hapa ya kiusalama katika taifa hili changa kuna watu wana yao ila wanatumia UKAWA kama kivuli tuu cha kutetea wanyonge na tatizo jingine lililojitokeza ni hiki chama kikuu cha upinzani CHADEMA kujiunga na marafiki asiowajua kiundani sasa sina budi na yeye nimweke kundi hilohilo na ajenda hizohizo kwasababu wote ni UKAWA.
Maswala madogo na marahisi ya kujiuliza ni haya hapa kwanini vuguvugu lao lianzie Zanzibar kule kwenye UAMSHO.?
Je walipokua Zanzibar hawa viongozi wa UKAWA tuna uhakika gani kama hawakukutana na UAMSHO.? Maana hapa kuna shutuma za CUF kua na uhusiano na UAMSHO.
Shutuma alizozitoa Lukuvi zina ukweli wowote? Maana Lukuvi ana kofia mbili huyu ya uwaziri na ujumbe sasa kama ni taarifa za kiintelejensia atakua nazo tu bila shaka.
Wameshindwa plan A je plan B watafanyaje au watakua ni kikundi cha waasi.?
Kuhusu kurudi kwa Sultan wa Oman vipi wameshakutana na Sharif kujadili.? Pia kuna taarifa za chini kwa chini kua hata PEMBA na UNGUJA zinavuguvugu la kujitenga kila mmoja kivyake, hata Nyerere aliliona na alishalionya mapema kama naongopa nikosoe. Pia kuna kauli fulani za wanzanzibar bungeni kama "Ya wazanzibar tuachie wenyewe tunajuana" hii kauli ni pana sana na ina maana kubwa.
CHADEMA ameungana rafiki asiomjua kiajenda aachane nao haraka sana hapo ni WORKING TIME BOMB.
Ushauri wangu kikundi cha UKAWA kifutwe tu nina wasiwasi kitakua kikundi kamili cha waasi kwanza siyo rasmi na wakiendelea na hujuma zao wachukuliwe hatua kali kabisa na kiitwe rasmi ni kikundi cha waasi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni