Ijumaa, 21 Machi 2014

JOHN DE MKALI. SHETANI NDANI YA TUSKER PROJECT FAME

Kipindi cha Tusker Project Fame ambacho ni kipindi kinachopigiwa mfano kama American Idols ni kipindi kinachokuza talanta za wasanii wapya na kimefanikiwa kuchezwa kwa misimu mitano kwa mafanikio.
Ajenda muhimu katika kipindi hiki ni kukuza vipaji vya musiki kanda nzima ya Afrika Mashariki.

Hii hapa list nzima ya washindi katika TPF kabla hatujaingia swala nyeti:
Msimu wa 1 Valerie Kimani
Msimu wa 2 Esther Mugizi
Msimu wa 3 Alpha Rwirangiza
Msimu wa 4 Hillary Davis Ntare
All Stars Alpha Rwirangira
Msimu wa 5 Ruth Matete
Msimu wa 6 Hope

Katika list tulioidondosha umeona kitu ambacho kimejitokeza?
Mastaa kuwa maskini kifedha na kiumaarufu. Jambo la mastaa hawa kushinda tuzo halafu kuwa maskini kwa muda mfupi haliwezi kuwa ni sadfa kwa mastaa hawa wote kwa mara moja. Lazima kuna kitu ambacho hakiko sawa hapa.

Victoria Kimani tangu ashinde tuzo imekuwa ni muhali kupata stori zake, wakati wa mwisho alipogonga vichwa vya habari ilikuwa wakati ambapo alikuwa na mapenzi ya chini na mwanamume aliyeolewa Erick Wainaina (mwanamziki nchini Kenya)

Ester Mugizi ambaye alikuwa na talanta ya juu na pia alikuwa akisomea musiki katika chuo kikuu hajulikani alipo wala hasikiki tena.

Staa wa Rwanda Alpha, ambaye alijulikana kuteka nyara hisia za mapenzi kwa madada zetu kwa sura na musiki inaonekana pia amejiteka nyara mwenyewe baada ya kushinda TPF. Jamaa huyu ndiye wa kwanza kutoonekana wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya nyimbo baada ya kudai kuwa sauti yake inamuumiza. Staa huyu talanta yake yote ya kumuiga Lucky Dube imepotea kabisa.

Davis, msanii mwingine wa kiganda ambaye alimulikwa na blogs nyingi kuwa amekuwa maskini baada ya mamanzi wa Nairobi kumdondoa hela ovyo alikuwa msanii mwenye talanta kuu. Msanii mwenye kucheza zaidi kumshinda Chris Brown, anauwezo mkuu wa kupiga gita kumliko Lucky Dube na kuimba zaidi ya R.Kelly...sahizi yuko wapi?

Ruth Matete, msanii wa Kenya kulikuwa na udaku usiokuwa na chanzo cha kuaminika kuwa alinaswa akitembea uchi barabarani. Lakini imedhibitishwa kuwa ilikuwa uongo tu. Mwanadada huyu sahizi anafanya kazi kuzindua albamu yake mpya na Universal Music Group. Amekuwa maskini, pesa amezikula zote.

Ok issue kuu hapa ni mbona washindi wa TPF wanakuwa maskini kimziki na kifedha baada ya mashindano hayo? Inasemekana kuwa eti chuo cha TPF hakiwapatii ushauri naswaha washindi hao jinsi ya kuendeleza vipaji vyao na mwishowe wanaanza kutumia pesa zao vibaya. Msanii kama Davis anaweza kutumia pesa hizo zote kwa madada na kujirusha, je staa wa kike Matete kwani kuliendaje? Hakutumia pesa zake kwa waume! Lazima kuna jambo ambalo haliko sawa hapa.

Soma K-Denk Wa TPF Ajiunga Na Kundi Pinzani La Kuiangusha Serikali 

Baada ya kujaribu kutaka jibu kwa swala hili zima, majibu yake yalikuwa ya kutatanisha. "Nenda katafute kwa mtandao wa Google kile kitu Michael Jackson alichosema, siko tayari kuuza roho yangu. Kwa vyovyote wanaweza kuchukua pesa zao ambazo tayari zimeshawarudia" mmoja wa washindi aliomba asitajwe jina wakati wa mahojiano na mwavuli wa bkuHABARI.

Kama tu mashirika mengine ya kimataifa ya wasanii, shirika la Afrika Kusini ambalo linawasajili washindi wa TPF linawahitaji washindi hawa kuweka mkataba wa kuuza roho yako kwa kundi la siri la Illuminati ili upate umaarufu na pesa nyingi. Bila hivyo utajiona ukiangamia kimziki na talanta yako yote kuipoteza. Pesa na umaarufu hauchukuliwi kwa nguvu bali vinachukuliwa bila wewe kuelewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni