john de mkali
Sasa hii ni mara ya 3 huu wimbo unatumika kimaslahi. Mara mbili zote zilizopita zilionyesha kama dada hakuambilia kitu licha ya watu wa pembeni kudaiwa kupiga hela ndefu..
Diamond, mshike mkono Saida. Wajanja wasije wakatumia tena ujanja wa makaratasi wakamlaza njaa.
Anga la burudani nchini hivi sasa lipo
kwenye msisimko wa tenzi ya Wasanii Diamond Platnumz na Raymond ambao
wameachia songi la Salome, ambalo ni marejeo ya songi pendwa
lililloimbwa mwaka 2000 na dada yetu wa Kihaya, Saida Karoli, liitwalo
‘Maria Salome’ almaarufu ‘Chambua kama karanga’..
Tumeona uongozi wa WCB chini ya Diamond ukijitoa lawama kwa kuonyesha
kuwa kuna makubaliano ya kuurudia huo wimbo baina yao na Dada Saida
kupitia menejiment yake.Sasa hii ni mara ya 3 huu wimbo unatumika kimaslahi. Mara mbili zote zilizopita zilionyesha kama dada hakuambilia kitu licha ya watu wa pembeni kudaiwa kupiga hela ndefu..
“Vyombo
vya habari vilikuwa vimeshanisahau, leo hii vinanitafuta,” anasikika
akisema Saida kwenye kipande cha sauti alichokiweka Diamond Instagram.
“Ndugu zangu baadhi wanajua hata sipo duniani, leo hii naona watu
mbalimbali wananitafuta, kwakweli nimefunguka, najihisi kuzaliwa upya,” alisema.
Maria Salome ulikuwa wimbo wenye mafanikio
makubwa kwa Saida Karoli. Pamoja na kumlipa kwa kuurudia wimbo huo,
Diamond amesema asilimia 25 za mapato ya wimbo huo yataenda kwa Saida
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni