Jumapili, 7 Desemba 2014

USIKU WA WAFALME DAR LIVE DIAMOND: NILISHAGANDISHWA NIGERIA SAA 8...john de mkali

DAR ES SALAAM,  Tanzania
BAADA ya kuchukua tuzo tatu kwa mpigo za Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video Awards (Choamva), staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, amefunguka ya moyoni na kusema kuwa alipokuwa nchini Nigeria alishawahi kugandishwa kwa saa 8 kisa kufanya kolabo.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Diamond aliyasema hayo alipokuwa na mazungumzo na waandishi wa habari yaliyofanyika katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni mara baada ya kuingia nchini akitokea Afrika Kusini kwenye tuzo hizo na kusema kuwa kuna kipindi alishawahi kuchekwa sana kutokujua Kiingereza lakini mwisho wa siku anaongea bila wasiwasi.
“Kiukweli nchini kwetu bado kuna watu hawapendi mafanikio, wakiona unatoka wataanza kukufanyia majungu.
“Ninachoweza kusema siwezi kukata tamaa hata siku moja na niwaambie tu nipo na nitapambana mpaka dakika ya mwisho.
Kuna wasanii wengi wakubwa nchi za wenzetu siwezi kuwataja majina, baada ya ushindi huu wa tuzo tatu walinifuata kwa nyakati tofauti wakitaka kufanya nami kolabo kati ya hao walionifuata kuna mmoja aliwahi kunigandisha nchini Nigeria saa tano asubuhi hadi kuonana naye saa mbili usiku kwa kunidharau,” alisema Diamond.
Kampuni ya Vodacom kwa kushirikiana na Coca Cola zinatarajiwa kumshusha Diamond na tuzo hizo, Desemba 25, mwaka huu ambayo ni Sikukuu ya Christmas ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, jijini Dar sambamba na kuangusha bonge moja la shoo.
Katika usiku huo uliopewa jina la Usiku wa Wafalme, mashabiki wote wa muziki wa Bongo Fleva watakaofika ukumbini hapo watapata nafasi ya kupiga ‘red carpet’ na kucheza na kuimba nyimbo zake zote kali kama vile Nimpende Nani, Nataka Kulewa, My Number One, Mdogomdogo, Bum Bum na hii ambayo ni habari ya mjini kwa sasa, Nitampata Wapi.
Mbali na Diamond, usiku huo utafunikwa pia na mfalme wa Taarab, Mzee Yusuf ambaye atapanda jukwaani na kundi lake linalotikisa kunako miondoko ya Pwani, Jahazi Modern Taarab na kupiga nyimbo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni