Ulikua unafahamu kwamba kuketi kwa muda mrefu ni hatari kwa afya yako? unaambiwa binadamu wa kawaida kwa sasa anakaa kwa muda wa saa nane mpaka saa tisa kila siku akiwa kazini, kwenye gari au nyumbani.
Ukiongeza saa nyingine 7 za kulala, inamaanisha unatumia robo tu ya muda wako ukiwa umesimama au ukiwa unatembea kwa siku ambapo muda huo mfupi wa kutuliza mwili unazidisha hatari ya unene lakini pia orodha ya maradhi mengine kama matatizo ya moyo, kisukari, saratani, magonjwa ya misuli, mgongo, mshtuko n.k
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Wanasayansi wanafananisha kukaa kama uvutaji wa sigara, ni kama mrundiko wa magonjwa ambayo hujionesha ukubwani.
Shirika la afya duniani limegundua kwamba kukaa bila kufanya kitu chochote ni chanzo cha nne kinachoua watu kwa kasi zaidi duniani ambapo pia ukiachana na kuongeza unene katika mwili imekua ikigharimu uchumi wa nchi ya Uingereza bilioni 145 kila mwaka kutokana na matatizo ya mgongo na misuli.
Shirika la afya duniani linashauri angalau kwa wiki mtu afanye mazoezi kwa dakika 150 ambazo ni sawa na saa mbili na dakika 40 ambapo ushauri mwingine ni wa labda dakika 30 kwenye siku tano, hiyo ni angalau kuliko kutumia muda mwingi kuketi ambako ni hatari kwa afya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni