Ilikua taarifa kubwa sana pale mtoto rubani mwenye umri wa miaka 17 alipotangaza maamuzi ya kusafiri na ndege ndogo ya injini moja kwenye nchi mbalimbali duniani ikiwa ni ndani ya Mabara matano, vituo 25 ndani ya nchi 15 kwenye siku 30.
Haris Suleman na baba yake mzazi ambae pia ni Rubani walichukua mafunzo mbalimbali ya kutua kwenye maji wakati wa dharura kabla ya kuanza safari yao waliyoiandaa kwa miezi wakiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa familia masikini nchini Pakistan waweze kwenda shule.
Sasa imethibitika kwamba mtoto huyu rubani aliekua anataka kuweka rekodi ya dunia kwa kuwa rubani mdogo aliesafiri umbali mrefu, amefariki dunia na mwili wake kupatikana baada ya ajali ya ndege hiyo iliyotokea baharini Jumanne usiku ambapo Baba yake ambae walikua pamoja hajulikani alipo.
Mpaka sasa chanzo cha kuanguka kwa ndege hii hakijajulikana ambapo Hiba Suleman ambae ni dada wa marehemu amesema ‘tunatumai baba yetu yu hai, tutaendelea kusali mpaka tutakapopata jibu la mwisho… ‘
Wawili hawa walikua na blog yao ambayo walikua wanapost vitu mbalimbali zikiwemo picha za wanakopita au kutembelea ambapo post yao ya mwisho kuiweka ilikua ni July 20 2014 Bali Indonesia.
Watu mbalimbali waliokua wanawafatilia wameanza kutoa salamu zao za rambirambi kwa familia baada ya kupokea taarifa za ajali waliyoipata ambapo mmoja wa waliokua wanawafatilia ni Private Pilot Ahmed.
Ahmed amesikitishwa na ajali waliyoipata na kusema imeuma zaidi hasa kwa sababu ndio ilikua karibu wamalize safari hii ambayo ni rekodi ya dunia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni