Tumekuwa waoga sana hata tunaogopa
kujadiliana ukweli, kila mtu anaogopa. Hii inaletwa na tatizo kubwa la
uchumi, uhakika wa ajira, kazi na biashara za kujuana, elimu mbovu
isiyoandaa watoto wetu kujitegemea.
Dodoma nyuso zote zilizobaki zinauwoga
mkubwa kuliko ukweli. Haya ndio madhara makubwa uchumi kushikiliwa na
serikali. Inasikitisha sana kumuona Dr mwenye PHD mwoga na muongo, sio
kwamba hajui anadanganya ila ni shida ndio inamfanya muoga na mwongo.
Rushwa za madaraka, ajira, biashara na tender za kujauna zinawafunga
wengi jela ya uhuru, ukweli, taaluma halisi na kuwajengea watanzania na
kizazi kijacho Tanzania njema.
Hatuwezi kutoka kwenye hili tope na
waoga hawa tulionao. Ili tuendelee kuna kizazi lazima kipumzike. Huwezi
kwenda mbele na askari anayegopa mabadiliko. Dunia inabadilika halafu
sisi tunahitaji kubakia pale pale.
Ukimsikiliza kwa makini Hotuma ya Rasimu
ya Jaji Warioba ilitoa mapendekezo mengi kuhusu muundo wa serikali,
haikujifunga ila kila muundo unahitaji mabadiliko makubwa. Kwanini wana
CCM hawataki kuujadili muundo wanaoupenda kwa kuzingatia maoni na
uwasilishaji wa Rasimu?
Kama kweli nia ni serikali mbili kwanini
wasiseme wazi, katiba ya sasa ya zanzibar is invalid, haipo
haitambuliki, wasiseme turudi kwenye seikali moja yenye nchi mbili?
Kwanini wasiseme mabadiliko yote yaliyofanywa kinyemela yamekiuka katiba
na hayatambuliki pande zote bara na visiwani?
Kwa nini wasikubali kujadili kwa kina
mambo yote yaliyouwa muungano wa serikali moja? Kwa nini wasijadili
ilikuwaje zanzibar ikawa nchi na katiba yake kinyume cha makubaliano ya
Muungano? Kwanini wasijadili kwanini Raisi wa Muungano sio raisi wa
Zanzibar tena?
Nataka Dr Mwakyembe mwanasheria, Andrew
Chenge, Nimrod Mkono, Werema, Sita, na wanasheria wote nguli wa CCM
waache mipasho warudie taaluma zao wapambane hoja kwa hoja. Yuko wapi
Asha Rose wa Migiro, Vijana wasomi kama Januari makamba, Mo, mko wapi
mnaogopa kuitetea serikali yenu kwa ukweli na uwazi?
Samweli Sita azuie mipasho , taarabu,
matusi, lugha za kebehi watu wajenge hoja na kushindana kwa facts.
Wananchi tusikilize wachambue ukweli, then tuambiwe tupige kura kutokana
na debate chanya.
Hata kama wafuasi na wajumbe wa chama
tawala hawataki, wajumbe wa Ukawa wamejipanga kwa data, facts, na jinsi
wanavyojenga hoja, Pamoja na kwamba wajumbe wa CCM wamebaki wenyewe
wameshindwa kushawishi umma kwa nini wanataka serikali mbili. Kama kweli
kina Mwakyembe wangekuwa na hoja za ushindi huu ndio ungekuwa muda wa
kushinda kwa hoja kwani wote wanatetea serikali mbili ndani ya mjengo.
Wananchi ni mashahidi wameshindwa wameishia kutukana hewa. Ukawa hawapo
ndani kila mchangiaji anatukana member ambao hawapo.
Leo hii kila anayesimama anatukana mtu.
Kama wanaCCM na wajumbe wao wangejua
hakuna katiba ya Ukawa wala ya CCM bali ya Tanzania, wasingeleta fujo na
kulazimisha kujadili rasimu ya CCM. Lazima tuijadili rasimu ya warioba
ama tuikubali kwa hoja ama tuikatae kwa hoja then tuipigie kura.
CCM wajipange wawape mijadala hii
wanaCCM wenye akili timamu na ufahamu ili wapambane na akina Lissu,
Zito, Kafulila, Lipumba, Mbatia, Jusa, nk. Team ya ukawa imejipanga
kiuchumi, kisheria, kijamii, kisayansi, kisiasa, diplomasia, nk nk. CCM
inabidi wa-copy jinsi ya kufanya kazi. Kusimamisha vidosho kuchangia
matusi na lugha za kubagua watanzania na uchochezi wa kijeshi haziwezi
kusaidia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni