Hatimaye ikulu ya Marekani imejibu ombi
lililotolewa na raia wa Marekani kwa Rais Barack Obama kumfukuza Justin
Bieber nchini humo, ombi lililopata sahihi takribani 275,000 ndani ya
siku 30 na kuvuka kiwango cha sahihi 100,000 zilizotakiwa kumfanya rais
alifikirie.
Katika tamko hilo, Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa haita-comment kuhusu ombi hilo linalojulikana kama ‘We ThePeople’.
Thanks for your petition and your
participation in We the People. Sorry to disappoint, but we won’t be
commenting on this one ...” Imeeleza katika tamko hilo.
Hata hivyo, imewashukuru watu hao kwa
kuonesha kujali kuhusu suala la uhamiaji na kwamba suala hilo
wamewaachia watu wengine walizungumzie.
“So we'll leave it to others to comment
on Mr Bieber’s case, but we’re glad you care about immigration issues.
Because our current system is broken."
Watu 275,000 walisaini ombi hilo kwa
madai kuwa Justin Bieber amekuwa mfano mbaya kwa vijana wa Marekani
kutokana na matendo yake mabaya ikiwemo uvutaji wa bangi, matendo ambayo
yalikuwa yakiripotiwa mara kwa mara huku akiripotiwa kuwa kero kwa
jirani zake.
Bieber amekuwa akikabiriwa na kesi kadhaa na nyumba yake kupekuliwa na polisi, huku akisimama kizimbani mara kadhaa kujitetea.
Hii ni petition hiyo iliyopata sahihi 275,000:
"We the people of the United States feel
that we are being wrongly represented in the world of pop culture. We
would like to see the dangerous, reckless, destructive, and drug
abusing, Justin Bieber deported and his green card revoked. He is not
only threatening the safety of our people but he is also a terrible
influence on our nations youth. We the people would like to remove
Justin Bieber from our society."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni