Ijumaa, 21 Machi 2014

JOHN DE MKALI. SHEIKH PONDA AZIDI KUSOTA

JITIHADA za Sheikh Ponda Issa Ponda, kutaka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ifanyie marejeo uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Oktoba mosi mwaka jana, zimegonga mwamba baada ya mahakama hiyo kulitupa ombi hilo.



Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Agustino Mwarija, ambaye alisema mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili na imefikia uamuzi wa kukubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa mahakamani na mjibu maombi ambaye ni Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, aliyetaka ombi hilo litupwe.

Februari mwaka huu, Feleshi aliiomba mahakama hiyo ilitupe ombi la Ponda, kwa sababu linakiuka matakwa ya Kifungu cha 372(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambacho kinakataza amri za muda, awali  zinazotokana na mahakama za chini zisikatiwe rufaa katika Mahakama za juu kama Ponda alivyofanya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni