YELEUUWI! Msanii asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amewatemea cheche wanaomnyemelea mpenzi
wake aliyemtaja kwa jina moja la Amani, akiwataka waache mara moja kwani akiwagundua atawatembezea kichapo.
Akipiga stori na mwanahabari wetu, Aunty Lulu aliweka ‘pleini’ kuwa ameshatonywa baadhi ya majina ya wanawake japokuwa hana uhakika kama ni kweli wanamnyemelea mumewe mtarajiwa ambapo akithibitisha kitachofuata ni mkong’oto kwani timbwili analiweza.
“Nampenda sana Amani, anachonipa hakuna anayeweza kunipatia, nimetulia, ameshanitambulisha kwa wazazi wake, ole wake nimnase mtu, atanieleza,” alisema Lulu.
GPL
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni